Ruka hadi kwenye maudhui makuu

ELIMU YA MUZIKI NA UZOEFU WAKE

P-Funk alikwenda kimasomo ya Mlio (sound) engineering kwa miezi 18 pale Amsterdam, Netherland kabla ajaingia kwenye kutayarisha muziki. Alikuwa anajua kitu anachotaka kufanya. Mwaka 1995 akiwa na vifaa vyake vichache alianzisha kampuni yake ya kurekodi muziki nyumbani kwake. Na ni katika kipindi hicho hicho neno ’Bongo’lilipokuwa linatawala katika misemo ya kiswahili cha mitaani na lilikuwa linaelezea hali halisi ya maisha ya Dar es Salaam na ndio kipindi hicho album ya Bongo ilipozinduliwa.

Akiwa bado ni mtayarishaji muziki mdogo, amefanikiwa kupata umaarufu katika fani ya muziki na hasa katika milipuko ya nyimbo zenye ladha ya Bongo.

Anakubali kuwa amepata utaalam na mbinu kutokana na kuwafanyia kazi watayarishaji wengine wa muziki wa Kitanzania kama Master J, Bonny Love na Rico. Mawazo yake na namna ya kuyaoainisha na muziki ndio hasa ambacho kinafanya muziki wake ufanikiwe.

Maoni