Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MASTER JAY

Master Jay

Fuatilia.........

Edit
Joachim Marunda Kimaryo (maarufu kama Master J; alizaliwa 9 Agosti 1973) ni muandaaji wa muziki nchini Tanzania.

Joachim Marunda Kimaryo
Jina Kamili
{{{jina kamili}}}
Jina la kisanii
Rap Master Jay, Master Jay, Baba Nuru nk.
Nchi
Tanzania
Alizaliwa
9 Agosti 1973
Aina ya muziki
Hip Hop, Bongo Flava, Kwaya, Dansi
Kazi yake
Mtayarishaji
Miaka ya kazi
mn. 1995 -
Ameshirikiana na
P Funk, Bonny Luv,Rajabu Marijani, Bizz Man, Marco Challi nk.
Ala
Kinanda,Guitar, Kinakilishi, Kuunjini Sauti
Kampuni
MJ Records
Master J amewahi kupata tuzo ya Kili Music Awards mara mbili, mwaka 2004 na 2006. Master Jay ana uwezo mkubwa sana wa utengenezaji wa muziki. Anamiliki studio tatu tofauti, moja ya muziki wa Kwaya, moja ya Bongo Flava na nyingine ya muziki wa Dansi.


ELIMU
Master J alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Upanga lakini aliishia darasa la PILI na kuhamishiwa Botswana baada ya familia yake kuhamishiwa nchini huko kikazi.

Mwaka 1996 alipata digrii ya electronics katika chuo cha City University Of London kilichopo bara Ulaya mbali na shughuli za kimuziki.

MUZIKI NA VIKWAZO VYA KIFAMILIA
Baada ya kupata digrii yake alirudi nyumbani na kuendelea na shughuli zake za kawaida pamoja na muziki, baba yake hakutaka kabisa mwanae ajishughulishe na muziki kiasi kufikia kutaka kumuachia radhi.

Pamoja na vikwazo alivyopewa na baba yake mzazi, Master J hakuacha muziki kwa kudai kuwa umo ndani ya damu yake.





Maoni