Kwanza alianza kwa kumpandisha chati Juma Nature, ambaye ndio nyota wa nyimbo za Bongo Flava, akaendelea kwa kutayarisha santuri ya Solo Thang, AY, Zay B, Sista P, Mike T, Ze Pungu, pia alishawahi kufanya kazi na Professor Jay alipotoa santuri yake mwenyewe. Pia amefanya kazi ya kutoa midundo kwa msanii Afande Sele au Selemani Msindi wa Morogoro mfano Nyimbo ya Simba Dume aliyoshirikishwa Feruz. Amefanya kazi na wasanii wengi wa Bongo wakiwamo Wakongwe Mr.II (2 Proud) a.k.a. SUGU, Monduli Mobb, Gangwe Mobb, Hop Pot Family akiongozwa na Soggy Doggy, Manyema Family. Mwaka 2019 Pfunk Majani amemuibua Rapcha (21), msanii anayechipukia katika muziki wa Afrika Mashariki akiwa na uwezo wa ku-rap pamoja na kuimba: ndiye msanii pekee aliyepo chini ya nembo ya Pfunk Majani kwa sasa.
Tarehe 20 Desemba 2019 Pfunk Majani aliachia wimbo chini ya Bongo Records unaoitwa "Moto Unawaka" akimshirikisha Rapcha, TkiLLA na Msamiati.
Maoni
Chapisha Maoni