Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Miikka Mwamba


 Miikka Aleksanteri Kari (amezaliwa tar. 16 Oktoba 1971, mjini Helsinki, Ufini) ni mtayarishaji wa muziki na mhandisi wa sauti toka nchini Ufini-Tanzania. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kitayarishaji kama Miikka Mwamba. Miikka Mwamba ni mtayarishaji mashuhuri sana kwa nchi ya Tanzania, na ameweza kujibebea umaarufu mkubwa sana nchini Tanzania kunako miaka ya 2000.

Miikka Mwamba.Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa
Miikka Aleksanteri Kari
Amezaliwa
16 Oktoba 1971 (umri 49)
Asili yake
Finland
Aina ya muziki
Hip hip
R&B
Dansi
Pop
Kazi yake
Mtayarishaji
Studio
Mwamba Productions
FM Studio
Kokwa Records
Tovuti

Mwambaproductions.com
Miikka aliwahi kufanya kazi na wasanii mbalimbali wa nchini Tanzania. Wasanii hao ni: Dully Sykes, Inspector Haroun, Lady Jay Dee, Mad Ice, Chegge, Mandojo na Domo Kaya, Solid Ground Family, Complex, Zahrani (maarufu kama Big Punisher wa Bongo), Only Face, Dknob na wengine wengi wa kutoka Tanzania.

Miikka Mwamba, ameshawahi kufanya kazi miaka mingi kwenye medani za muziki, filamu, michezo ya kuigiza na dansi, ni swala ambalo si mara nyingi kufanyika kwa nchi ya Ufini na Tanzania pia.

Miikka alihitimu elimu yake ya msingi na secondary katika Lohja, ambacho ni chuo cha sanaa (Torkkelin kuvataidelukio) alisomea Helsinki, na shahada ya uzamili (MA) alipata Theatre Academy of Finland, Dept. of Light and Sound Design.

Nyimbo zilizotamba Edit
Julieta - Dully Sykes (2000)
Athumani Mlevi - Solid Ground Family (2001)
Baby Gal - Mad Ice (2002)
Tupa Mawe - Zahrani na Complex (2001)
Twenzetu - Chegge, Ferouz na Mh Temba (2005)
Elimu Mitaani.com - Dknob (2003)
Kitu Gani - Dknob (2007)
Viungo vya Nje Edit
Tovuti ya studio ya Miikka Mwamba Archived 21 Novemba 2008 at the Wayback Machine.
Maelezo binafsi kuhusu Miikka Mwamba katika faili ya PDF[dead link]

Maoni